Hamisa Mobetto Ampindua Kibabe Wema Sepetu


Miaka ya Nyuma Kidogo Kabla ya Instagram kuchanganya Sana, Wema Sepetu ndio alikuwa Superstar Wakike Pekee Tanzania Nzima, kila siku Magazeti, blog, Website, Facebook ziliandika mambo kibao kuhusu Wema Sepetu.

Wema sepetu ndio alikuwa Queen wa Drama Hapa Tanzania, Mara Leo video Zimevuja akidendeka, Mara Kakamatwa na Bangi, Mara skendo kuwa anafuga Mashoga na Wasagaji, mara anadate na Muheshimiwa Fulani, mara yule mara huyu. Yani tulikuwa hatupumui, kila siku sepetu sepetu.

Ila Hivi sasa Mambo ni tofauti, kila zama zina malkia wake, kwasasa Malkia ni Hamisa Mobetto, Leo hii Hamisa akinywa maji watu wanapost, akikohoa watu wanapost, akicheka inakuwa story kubwa , akikiss sasa, Mpaka Blog za udaku za nje zinapost, yani ukijumlisha na Mitandao ya kijamii ilivyopamba moto basi Story zake zinazagaa kila mahali.

Umaarufu pamoja na Ustar wa Wema Sepetu/Hamisa Mobetto kwa kiasi kikubwa Chanzo chake ni Uhusiano wa mapenzi kati yao na Diamond, Kila mmoja kwa wakati wake alipodate na Diamond umaarufu na Ustar uliongezeka kwa kiasi kikubwa, Sio kwamba hawakuwa maarufu, ila nachomaanisha hapa Ni kwamba umaarufu wao ulizidi kupindukia.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post