Hamisa Mobeto Ajibu Kumkomoa Diamond Platnumz "Sijawahi Kumuwaza Hata SIKU Moja"




MWANAMITINDO wa kimataifa na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amejibu madai kwamba amekuwa akionekana na mastaa wakubwa duniani kwa lengo la kumkomoa baba mtoto wake, Diamond Platnumz.


Mobeto anasema kuwa, kwa kawaida yeye huwa hana matatizo yoyote na mpenzi wake yeyote wa zamani.

Mama huyo wa watoto wawili anasema, hafuatilii maisha ya wapenzi wake wa zamani wala hajali kuhusu wanawake
wanaochukuliwa na maeksi wake na hana kinyongo chochote dhidi ya mpenzi wake yeyote wa zamani.


“Mimi ni mpenzi wa zamani asiye na matatizo. Mimi ni ex ambaye siwezi kujali kuhusu kile unachofanya sasa hivi


“Huwa najali cha kwangu kwa muda wangu. Ikitokea kwamba tumeachana, hayo yameisha. Siwezi kujali ukiwa na mwanamke mwingine na sidhani kama nimewahi kujali kwa ex wangu yeyote akiwa na mwanamke mwingine.


“Naamini kwamba kila kitu kinatokea kwa sababu ni chema, kitu kikija kwako ni cha kwako. Kama siyo cha kwako, basi siyo cha kwako.


“Pia naamini watu huchumbiana na kuachana, mkiachana inamaanisha riziki inaishia hapo au Mwenyezi Mungu alitaka ufike hapo uendelee na safari.



“Mimi sijawahi kumuwazia ex wangu yeyote yule vibaya. Sijawahi kufanya kitu kwa ajili ya yeyote yule. Huwa nafanya mambo yangu na kufanya yale yanayonifurahisha,” anasema Mobeto


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post