Faida (5) za Kuwa Katika Mahusiano na Mwanaume Mfupi





Linapokuja suala la mahusiano, wanaume wenye kimo cha kiasi fulani hupata mtihani kidogo katika kuanzisha mahusiano.

Baadhi ya wanawake huona wanaume wafupi hawana mvuto au wenye viburi, lakini hii inatokana na mazoea ya kwamba mwanaume kwenye mahusiano ni lazima awe mrefu liko mwanamke kitu ambacho hakina ukweli ndani yake.

Kuwa na mahusiano na mwanaume mrefu sio jambo baya, ila jambo baya ni kumkataa mwanaume kisa kimo chake, pasi ya kuwa na sababu yeyote ya msingi. Lakini, habari ni kwamba yapo ambayo mwanamke anaweza kuyakosa kutoka kwa wanaume wafupi. Mambo hayo ni kama yafuatayo.

1. Kujiamini na Kujikubali
Mwanaume mfupi mwenye uwezo wa kuwa na mwanamke mrefu katika mahusiano, akawa na furaha bila kujali chochote, ujue kiwango chake cha kujiamini sio cha kawaida. Mtu huyu maana yake amemudu kutoona kimo chake kutokuwa kikwazo cha yeye kufanya yale yampayo furaha.


 
Kawaida imewajenga watu wenye uhaba wa kimo kuwa na fikra mbaya juu yao kwenye suala la mapenzi, fikra hii huwarudisha sana nyuma

2. Uauminifu
Utafiti uliofanywa na Ashley Madison ulionesha kuwa wanaume warefu ni rahisi kufanya usaliliti mara mbili zaidi kuliko wanaume wafupi. Kwakuwa jamii ina taswira na mawazo mabaya juu watu wafupi, hivyo usumbufu wa hapa na pale kutoka kwa wanawake unapungua kwao, hivyo kupunguza uwezekano wa wao kufanya usaliti.

3. Sekta ya kufanya mapenzi
Utafiti uliochapishwa na jarida la Journal of Sexual Medine unaonesha kuwa wanaume wafupi ni hodari sana katika sekta ya kufanya mapenzi. Lakini jaridi hilo linaonesha kuwa wanaume wafupi hufanya mapenzi muda mrefu kuliko wafupi, kwanza hudumu kitandani, pili huweza kufanya mara nyingi kwa siku zaidi ya wanaume wafupi.


Sababu ni kwamba wanaume wengi wafupi huhisi pengine kutokuwa na urefu inaweza kuwa sababu ya kuachwa, ili kulinda hali hiyo isitokee, basi hujiimarisha katika sekta fulani (ngono) na kuhakikisha anakuwa vizuri ili hata mwanamke akitaka kuondoka akose sababu.

4. Uvumilivu
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha New York unaonesha kuwa wanaume warefu hupata huoa haraka kuliko wanaume wafupi, lakini ajabu ni kwamba watu wafupi pale wanapoingia kwenye ndoa, ndoa zao hudumu zaidi kuliko watu warefu.

Hii inatoka na uvumilivu wao katika kustahamili mambo, hii ni tofauti na wanaume wengi warefu, kiwango chao ch uvumilivu ni kidogo hivyo kupelekea talaka nyingi.

5. Viatu virefu, basi tena!
Viatu virefu ni adha, miguu kuuma na karaha zote za viatu virefu zitapumzika ukiwa na mahusiano na mtu mfupi. Mkifanya mtoko wa chakula cha usiku au mchana hutolazimika kuvaa viatu virefu, kwani ili kupendeza na kuwa na muonekano mzuri mbele ya macho ya watu (japo sio lazima), unaweza kupumzisha viatu vyako virefu kwa muda


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post