Erick Omondi Aendelea Kupambania Mziki wa Kenya Atoa Hutoba Kwa Taiga Tanzania Tumetajwa


Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya Erick Omondi, ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuzungumza na mashabiki wake kuhusu mapambano yake dhidi ya kuirudisha hadhi ya muziki nchini humo.

Mazungumzo aliyoyaita hotuba kwa taifa, ambapo Omondi alikaririwa akisema kuwa yeye ni mtu mwenye ushawishi na nguvu kubwa Afrika Mashariki, na ndio sababu ya kujihusisha na harakati mbalimbali za ukombozi wa Sanaa ya Kenya inayoonesha viashiria vya kutumbukia shimoni

"Nina ushawishi mkubwa nina imani na harakati zangu za kuufanya muziki wa Kenya kuwa mkubwa tena." Alisema Omondi

Kwa takribani mwezi mmoja uliopita, Omondi amekuwa na mzozo na wasanii, si wa ndani ya Kenya tu bali kimataifa pia, hii imechagizwa na ujio wa tamasha la Desemba 12, AFRO-VASHA litakalopambwa na baadhi ya wasanii kutoka nchini Tanzania akiwamo nyota wa muziki wa Bongo Fleva Alikiba na Harmonize.

Kufuatia kampeni yake ya kutaka wasanii wa kenya wapewe kipaumbele zaidi ya wasanii wengine kutoka nje ya taifa hilo,Omondi aliwataka Wakenya kususia tamasha hilo, ikiwa waandaaji hawatatii ombi lake la kubadilisha Mabango yanayowaonyesha wasanii wa Kenya kama bidhaa ndogo sokoni na wageni kuonekana wenye thamani zaidi.

"Ninatoa wito kwa kila Mkenya kususia tukio hili. Waandaaji hawa ni wachafu na wanadharau sana, tulikubaliana kwamba hatuhudhurii hafla yoyote ambayo inadharau juu yetu, kwa nini Super stars wetu wanawekwa katika mabango haya kama kama wasanii wadogo zaidi," aliandika Eric Omondi kwenye ukurasa wake wa Instagram muda mfupi baada ya kumaliza kuzungumzo yake kupitia IGTV.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post