Dully Sykes Amjibu Harmonize "Umenikosea Sana Uliposema Nimetumwa na WCB Nikuchafue"



Baada ya Msanii Harmonize kufanya mahojiano na kuzungumza kuhusu Mkongwe kwenye Game ya muziki wa Bongo Fleva @princedullysykes kuhusishwa kutumwa ili kumshtaki kwa kuiba wimbo wake Msanii huyo ametolea ufafanuzi .

Star huyo amefunguka kwenye mahojiano na @millardayo kuhusu tuhuma hizo akieleza kuwa Hajawahi kuwa mtumwa na hawezi kuwa mtumwa mpaka anakufa " Dully Sykes ametumia nafasi hiyo kutolea ufafanuzi kwamba WCB ni familia yake kama familia za wadogo zake wengine kwenye muziki zikiwemo media zote huku akidai hawawezi kumtuma kumdhihaki mtu .

Dully Sykes ameweka wazi kuwa ametumia muda mrefu kujenga Heshima yake na kama kuna mtu anafikiria kuwa yeye anatumwa kumdhihaki mtu atakuwa amemkosea .


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post