Aliyekuwa Dereva wa basi la Sharon lililosababisha ajali na kupelekea vifo vya Askari Polisi wanne mkoani Njombe na majeruhi saba William Emmanuel (28) amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela na kufungiwa leseni yake kwa muda wa miaka miwili.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi Njombe Liad Shamshama akiwa na Wakili wa Serikali Andrew Mandwa amesema tukio hilo la ajali lilitokea mwaka jana mwezi Februari maeneo ya mlima wa polisi barabara kuu ya Njombe Songea saa 12 alfajiri.
Amesema siku ya tukio dereva huyo alikuwa akiendesha basi aina ya Youtong alipofika maeneo ya mlima wa polisi alilipita gari jingine sehemu ambayo haikutakiwa kufanya hivyo na kuligonga gari la polisi aina ya Land cruiser na kusababisha vifo vya askari hao.
Askari waliofariki kutokana na ajali hiyo ni Marianus Hamis Saidi, Heri Athumani Soka, Michael Ernest Mwandu na Dickson Kagoda Maijo.
Post a Comment