Rapa na muigizaji wa filamu ya ‘Power’, 50 Cent amemuomba radhi muimbaji na muigizaji mwenzake, Madonna baada ya Madonna kutofurahishwa na utani alioufanya rapa huyo juu ya picha yake.
50 Cent aliikejeri picha ya Madonna ikimuonesha yupo chini ya uvungu wa kitanda huku akiwa na nguo ya ndani, rapa huyo aliifananaisha picha hiyo na tukio moja lililotokea katika filamu ya ‘Wizard of Oz’ jambo ambalo lilimkasirisha Madonna.
Kupitia mtandao wa Instagram kwenye Insta story, Madonna aliandika maneno yaliyoonyesha kukasirishwa mno na kitendo alichokifanya 50 Cent huku akiambatanisha na picha ya zamani ikiwaonesha wawili hao wakiwa pamoja, Madonna aliandika : ‘’Huyu ni 50 Cent akijifanya kuwa ni rafiki yangu.
Sasa umeamua kuniongelea vibaya, nadhani kazi yako inazingatiwa kwa kuwadharirisha wengine kwenye mitandao ya kijamii!’’ Madonna aliendelea ‘’Una wivu tu, hutoonekana bora kama mimi na wala hutopata mashabiki wengi kama mimi ukishafikia umri wangu’’
Kufuatia maneno hayo 50 Cent naye ameandika maneno ya kuomba msamaha kupitia mtandao wa Twitter , ‘’Lazima nitakuwa nimemuumiza Madonna, alienda na kuchukua picha ya zamani ya MTV ikituonesha tupo pamoja. Ok! samahani sikukusudia kukuumiza, sifaidiki na hii kwa vyovyote vile bali nilisema kilichokuja akilini mwangu nilipoona picha yako kwa sababu ya mahali nilipoiona hapo awali, natumai utakubali ombi langu la msamaha’’
Madonna hajaongea chochote juu ya ombi la msamaha kutoka kwa rapa 50 Cent.
Post a Comment