Wafukua Kaburi la Albino na Kutokomea na Mguu Mmoja wa Kulia...


Jeshi la Polisi mkoani Tanga, linawashikilia watu watatu wa familia moja kwa madai ya kufukua mwili wa kijana mwenye ualibino, Heri Kijangwa (45), kisha kutoweka na jeneza pamoja na mabaki ya mwili wake ikiwemo mguu wake wa kulia.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na majina ya watu hao yamehifadhiwa kwa sasa.
“Tunaendelea na uchunguzi kubaini kama kutakuwa na watu wengine wameshiriki, tunataka kujua sababu za kufukua mwili huo na tunataka kujua mabaki ya mwili huo wamepeleka wapi,” alisema.
Mwishoni mwa wiki, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la Under the Same Sun nchini Canada, Peter Ash, alitoa taarifa kwa umma kulaani tukio hilo na kueleza kuwa Heri alifariki Julai 4, mwaka huu kutokana na saratani ya ngozi na mwili wake ulizikwa Julai 7, Kijiji cha Tandwa, wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

Ilifafanua kuwa Oktoba 26, mwaka huu, familia ilikuta kaburi limefukuliwa na watu wasiojulikana wakachukua jeneza pamoja na mabaki ya mwili wake.


Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>

“Eneo la kaburi hatujakuta jeneza wala mabaki ya mwili wake. Tunalaani kwa nguvu zote tukio hili tunaiomba serikali kufanya uchunguzi na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya uhalifu huu nchini,” alisema na kuongeza;
“Pia tunaiomba Serikali ya Tanzania kuongeza jitihada za kudhibiti saratani ya ngozi kwa kundi hili. Heri alikuwa ni mnufaika wa programu zetu za elimu, tunasikitika sana kwa unyama huu,” alisema.

Ash alisema Under The same Sun walimsomesha kijana huyo na kabla ya mauti alikuwa anachukua Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, akiwa amemaliza shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kimataifa na Teknolojia mwaka 2015.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post