Katika machawa wote Tanzania, BabaLevo ndio hajielewi na anavuka mipaka ya Uchawa wake, mwijaku na na @h.baba_ nao ni chawa lakini uchawa wao uko smart sio kama uchawa wa kijinga wa @officialbabalevo . Sometimes msanii lazima uwe na wapambe wako lakini wasivuke mipaka, huyu mpambe wa Diamond anazingua sana.
Haiwezekani kila siku anatumia lugha mbaya kumchafua harmonize na jitihada zake, Harmonize mwenyewe anakiri kwamba ni mtoto kutoka katika familia maskini, anapambania ndoto zake, lakini anatokea chawa mmoja anaanza kumkatisha tamaa.
Mambo anayofanya babalevo hayaendani na Umri wake, baba levo angechelewa kidogo tu angemzaa harmonize, sasa ni aibu kubwa sana Kwa Mtu mzima kama babalevo kugombanisha vijana wa kitanzania wanaojaribu kupambana kutafuta pesa na kuitangaza Tanzania kupitia muziki wao.
Babalevo anafanya huu ujinga lakini watu wanafumbia macho. @rayctanzania ameshatabiri kwamba bifu hili la harmonize na diamond litaishia pabaya, na ikitokea hivyo wa kuwajibishwa wa kwanza ni babalevo na kundi lake maana wao ndio wanachochea moto.
Wadau wa sanaa Msifumbie macho jambo hili, muziki bila machawa wa kuchafua wasanii wengine unawezekana. Rayvanny alichukua BET, Je alikuwa na chawa wake? Tangu hawa machawa waibuke Wanamuziki wa Tanzania wamepata faida gani?
By @hopetygatz
Post a Comment