Usijaribu kumtesa Pasta Lucy, Ringtone achomwa na gere akimuonya nabii Muhindi



Muimbaji wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ni miongoni mwa wanaume wengi ambao wamevunjika moyo baada ya Pasta Lucy Natasha kumtambulisha mpenzi wake.


Pasta Lucy Natasha aliposwa na Nabii Stanley Carmel, jioni ya Jumamosi, Novemba 27, 2021.

Hafla hiyo maridadi ilihudhuriwa na jamaa na marafiki akiwemo mama yake Natasha, pasta Wanjiru na wadogo wake.

Watu tajika Kenya akiwemo Maina Kageni, Mike Sonko, Emmy Kosgei na Lillian Muli, walimtakia heri njema Natasha na Carmel katika ndoa yao.


"Amefanya kila kitu kizuri kwa wakati wake. Mhubiri 3:11. Hongera ❤️ binti yangu Natasha May Heaven akuheshimu milele," kasisi Wanjiru alichapisha akiambatanisha pamoja na picha za Natasha na mpenzi wake.

Ringtone akoroma
Katika ujumbe wenye mada 'Barua ya onyo', Ringtone alisema:

“Bwana Carmel ujumbe huu ni wa kukuonya Lucy Natasha anapendwa na wengi hapa Kenya na hakukuchagua kwa sababu amekata tamaa,” alisema.


"Wanaume wengi wameumia mioyoni mwao kwa sababu alikuchagua wewe kuliko wanaume wengi matajiri na wazuri kama mimi. Usimfanye dada yangu alie," aliongeza.

Ringtone alimwarifu mhubiri huyo wa India kuwa tayari kwa hafla kubwa ya harusi na kuanza kukopa mikopo iwapo hana pesa za kutosha

Alitishia kurudisha pete ambayo alimupa mhubiri huyo mrembo.

"Nenda utafute pesa ukafanye harusi kubwa. Ukiwa umefeli, ukakope mkopo ama sivyo tutakurudishia pete yako ya uchumba," alisema.


 
Muimbaji huyo wa wimbo Pamela pia alimtaka Carmel kuboresha maisha yake iwapo yuko kwenye kiwango cha chini kumliko Natasha.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post