Ujumbe wa Samia kwa Serikali ya China



Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya China kwa kuwa bega kwa bega na Serikali ya Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.


Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 14,2021 katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya jengo la chuo cha Taifa cha ulinzi iliiyofanyika jijini Dar es Salaam.


“Watu wa China wamekuwa marafiki, wadau na washirika wetu muhimu katika shughuli za maendeleo. Makabidhiano haya tunayoyashuhudia yana akisi nia yao njema ya kushirikiana nasi,  kwa niaba ya Watanzania wote nipende kuishukuru sana  Serikali ya China kwa msaada wenye kuweka alama,” amesema.


Ameeleza ujenzi wa chuo hicho utalisaidia jeshi la polisi na nchi kwa ujumla kuokoa fedha nyingi iliyokuwa ikitumika kusomesha wanafunzi nje ya nchi na sasa wanafunzi hao wanaweza kuyapata mafunzo hayo nchini.


“Hivyo gharama ambayo ingetumika kuwapeleka wanafunzi nje ya nchi itatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo,”amesema.


Hivyo Rais Samia amesema ni jukumu la Taifa  kuhakikisha chuo kinatimiza malengo ya kujengwa kwake ikiwa ni pamoja na kutoa wito kwa walimu kujituma katika ufundishaji wao.


ADVERTISEMENT

“Ninatumaini mtatumia fursa hii kuongeza wigo wa mafunzo mnayoyatoa kwani hiki ni moja kati ya chuo kimojawapo mashuhuri,”amesema.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post