Gari moja katika jimbo la California, Marekani liliibua tukio la kushangaza baada ya moja ya mlango kufunguka na kumwaga mamilioni ya dola iliyotapakaa chini.
Katika tukio hilo la Ijumaa, Novemba 19, msongamano ulishuhudiwa California huku watu wakikimbia kuokota pesa.
Akirekodi kisa hicho, mwanamke ambaye anatambuliwa kwenye Instagram kama Demi Baby, alisema hajawahi kuona tukio la kushangaza kama hilo.
Sehemu ya video hiyo ilimuonyesha mwanamume mmoja akiwa amejaza mabunda ya noti ya dola mikononi mwake akiwa amejawa na furaha.
Hata hivyo, Fox News inaripoti kuwa watu kadhaa ambao waliokota pesa hizo walikamatwa.
Nairobi: Jamaa Afariki Dunia Baada ya Kupigwa na Keyateka Kufuatia Mzozo wa Kodi
Kulingana na ripoti ya NBC News, FBI ilifichua kuwa japo baadhi ya watu walirejesha pesa hizo, wengine walionyeshwa wakihepa na pesa za wizi.
Maoni ya wanamtandao:
tony.frank_ alisema: "Jambo hili la fadhili linahitaji kutokea kwa 9ja kufanya niangalie kitu."
ice_rum_ alitania: "Angalia jinsi wote walivyoegesha ili kusaidia kuondoa fujo barabarani, ubinadamu adimu sana."
boudicca__london alisema: "Kwa nini wanarekodi na hawataki kuchukua pesa."
milly_posh21 alisema: "Badala ya wewe kuchukua pesa unafanya mahojiano."
samspedy alisema: "Mungu wa Nigeria, tafadhali usitupunguze."
Jamaa awatupia watu pesa
TUKO.co.ke iliripotia awali kuhusu video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha jamaa akiwa katika msafara wa magari akiwatupia watu pesa.
Gari la kwanza katika msafara huo lilikuwa na watu waliokuwa wameninginia upande mmoja.
Na lingine lilikuwa na jamaa aliyekuwa amepanda juu ya gari akiwarushia watu pesa na gari lingine lilifuata likiwa na watu waliokuwa wakishangilia kitendo hicho.
Post a Comment