Soko Maarufu Kenya la Gikomba Nairobi Laungua na Moto



Moto umechoma upande mmoja wa soko la Gikomba jijini Nairobi na kuharibu mali ya thamani isiojulikana mapema Jumatatu. Saa 48 kabla, wafanyabishara walipata pigo baada ya huduma ya jiji la Nairobi kupatiwa ruhusa na mahakama kuwaondoa baadhi ya wauzaji mitumba ili kutoa nafasi ya upanuzi wa kituo cha afya cha Pumwani Majengo Health Center.



Eneo la soko lililochomeka lilikuwa lile la mitumba ambapo wafanyabiashara wengi uhifadhi mali yao.

Wafanyabiashara waliowasili walikuwa tayari wamechelewa kuokoa mali yao huku ikiwa ni mabati yaliochomeka pekee ndio yaliosalia.

Gari la huduma ya Zima moto la jiji la Nairobi liliwasili katika eneo la tukio lakini moto huo tayari ulikuwa umesambaa kutokana na vibanda vya mbao vilivyotengenezwa .



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post