Mwanamama Shilole amekwaa skendo ya utapeli na kulazimika kuwajuza mashabiki wake wote kuwa hahusiki na akaunti yoyote katika Mtandao wa Facebook wala hajatangaza nafasi ya kazi sehemu yoyote.
Shilole anasema kuwa, kwa taarifa zozote kuhusu habari zake atatoa kupitia katika ukurasa wake rasmi wa Instagram ambao una tiki ya bluu.
Shilole ameandka; “Nasikitika sana kwa watu ambao wanatumia vibaya mitandao, pamoja na jina langu kwa lengo la kuwatapeli wengine.
“Kwa sasa sijatangaza nafasi yeyote ya kazi, na ukurasa huo sio wangu. Swala lolote linalotoka kwangu litaonekana kwenye kurasa zangu rasmi, hapa Instagram ni @officialshilole na Facebook ni Shilole na account zote ziko verified (zina kitiki cha bluu).
Hivyo usikubali kudanganyika na watu wote wanaotumia jina langu isivyo halali.
“Nitafuatilia kwa ukaribu ili sheria na vyombo husika viweze kuchukua hatua..”
Cc; @sifaelpaul
Post a Comment