Rapper P Mawenge Awasaliti Kikosi Kazi, Adai Weusi Ndio Kundi Bora la Hip Hop Tanzania




Msanii wa Hip Hop nchini na member wa kundi la muziki la Kikosi Kazi, @pmawenge ameachia wimbo unaitwa Nahamia Weusi kitu ambacho kimeleta maswali kwa mashabiki wengi wa muziki hasa wa Hip Hop ambao wanaelewa wazi Battle la Kikosi Kazi na Weusi kwenye hili game. Kwanini imekuwa hivi kwa P Mawenge, na kwanini hasichukuliwe kama snitch kwa wanae?

Akiwa kwenye Empire ya EFM,P Mawenge ameeleza sababu za Nahamia Weusi,akiwataka watu kuwa inabidi waelewe Kikosi Kazi na Weusi hawana uhasama wowote ule, hivyo hizo battle za kwenye muziki zisichukuliwe kuwa watu hawa hawawezi kukaa pamoja kwenye maisha ya kawaida au kufanya collabo kwenye muziki.

Sababu nyingine, P Mawenge amedai kuwa ukiacha kushambuliana kwenye nyimbo zao, ila huwezi kubisha kuwa Weusi sio kundi bora zaidi kwa sasa,akidai si kila kitu cha kupinga vingine vya kuiga,weusi wameweza kuliimarisha kundi lao na kulifanya kundi kubwa kwenye huu muziki bila kuvurugana, na wamedumu kwa muda mrefu kitu ambacho makundi Mengi yamefeli. Hivyo weusi ni kundi bora kiuendeshwaji ila Kimichano, Kikosi Kazi ndio Mateacher wao


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post