Picha ya Wapenzi Yauzwa Bilioni 80




Mchoro wa picha ya wanandoa wawili inayojulikana kwa jina la “Diego and I” iliyochorwa na mchoraji maarufu kutoka America Kusini, Frida Kahlo, imeuzwa kwa Dola za kimarekani Milioni $34.9 ambazo ni sawa na Bilioni 80 za kitanzania kwenye mnada uliofanyika huko jijini New York, na hivyo kuweka rekodi ya kuwa picha ghari zaidi duniani kuwahi kuuzwa kutokea Amerika kusini.

Picha hiyo inaelezea uhusiano wa kimapenzi kati ya “Frida Kahlo” na mumewe “Diego Rivera” ndio sababu ikaitwa (“Diego and I”), ambapo wakati wa uchoraji wa picha hiyo inaelezwa kuwa kulikuwa na uvumi ulienea kwamba Diego alikusudia kumuoa nyota wa filamu Maria Felix, ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Ingawa hakuna kilichotokea na hivyo Diego alibaki na Frida, kutokana na uvumi huo Frida aliumia na ndio sababu ya kuamua kuchora mchoro huo ambao ulikamilika miaka mitano kabla ya kifo chake mnamo 1949.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post