Pablo: Kila Mtu Atacheza Kwenye Kikosi Changu




KOCHA mkuu wa Simba, Pablo Franco ameweka wazi kuwa anataka kuona kila mchezaji wa timu hiyo anapambana kuhakikisha anafanya bidii mazoezini na kila anapopewa nafasi kwa kuwa amepanga kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza.

 

Pablo jana Jumapili aliiongoza Simba kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

 

Tangu atangazwe na Simba kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Pablo amefanikiwa kuiongoza Simba katika michezo miwili ya kimashindano rasmi dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba walishinda mabao 3-1 na mchezo wa jana Jumapili.



Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Pablo alisema: “Tuna kikosi kipana na wachezaji wenye ubora wa kutosha, imani yangu ni kwamba kila mchezaji aliye ndani ya klabu hii hayupo hapa kimakosa bali anapaswa kuisaidia klabu hii.

 

“Hivyo nimekaa na wachezaji wote na kuwaambia kuwa nataka kuona wanajituma mazoezini na kila wanapopata nafasi ya kucheza kwa kuwa kila mchezaji atapewa nafasi ya kucheza na kuonyesha alichonacho.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post