Ni Noma na Nusu Album ya Harmonize Yakamata Namba Moja Apple Music


Ikiwa bado haijatimiza siku moja, album mpya ya msanii @harmonize_tz "High School" yajiwekea rekodi ya aina yake kupitia Apple Music.

Tangu iachiwe usiku wa kuamkia leo, tayari ina saa 6 lakini imefanikiwa kuchumpa na kuingia kwenye Top Albums za mtandao wa Apple Music Tanzania.

Album hiyo yenye jumla ya ngoma 20, inakamata namba MOJA huku ikiiacha nafasi tatu album ya Ed Sheeran 'Equals'. Nafasi ya pili anaikamata Alikiba na album yake 'Only One King' na nafasi ya nne imekaa EP ya Rayvanny, 'New Chui'.

@harmonize_tz ambaye ni Mkurugenzi wa lebo ya Konde Gang, kwasasa anashikilia rekodi hiyo Apple Music na hili linadhihirisha kuwa "High School" inaendelea kifanya vizuri kupitia mtandao huo.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post