Rapper @naytrueboytz ameeleza kuwa msanii #Kusah ni msanii mzuri sana ,lakini watu wanashindqa kumzingatia kwa sababu ya mambo yake ya mahusiano.
Ney amefunguka hayo kupitia insta story yake, akieleza kuwa hata yeye humsikiliza sana msanii huyo, lakini watu wanashindwa kumzingatia kwakua anaonekana king'asti (mtu wa kulelewa kwenye mahusiano) na kama hayupo serious na muziki wake, huku mahusiano yake yakiwa na promo kubwa kuliko.
Aidha rapper huyo amemaliza kwa kumahauri msanii huyo kuchagua moja kati ya mahusiano ama mziki wake kwakua bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwenye muziki.
✍🏾@keviiiy.iam
Post a Comment