Staa wa filamu za kihidhi Boll, Sanjay Dutt @duttsanjay amesema hakuna sehemu bora duniani kama Tanzania ambayo unaweza kutembelea na kuwekeza.
Sanjay Dutt ambaye ametamba na filamu mbalimbali tangu miaka ya 80 na kuchukua tuzo tofauti, yupo nchini tangu juzi Novemba 6, 2021 na amekutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa. Akizungumza baada ya kuwasili nchini, amesema siku zote amekuwa akimuambia kila mtu kuwa hakuna sehemu bora na nzuri kama Tanzania.
HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL APP, DOWNLOAD HAPA UWE NAYO KWA SIMU YAKO..USIPITWE
“Tanzania ni kama nyumbani kwangu, nimekuwa nikimuambia kila mtu nchini kwangu na hata Marekani na Uingereza kuwa hakuna sehemu bora duniani kama Tanzania, unaweza kuja kutembea, pia unaweza kuwekeza,” amesema Sanjay Dutt.
Ikumbukwe, hii si mara ya kwanza @duttsanjay kutembelea Tanzania mara ya mwisho ilikuwa 2017.
Post a Comment