Mwanamke Ashambuliwa na Fisi Baada ya Kukataliwa na Aliyepaswa Kuwa Mwajiri Wake



Irene Mbithe alikuwa akisafiri hadi Mombasa kwa kile alichodhania kwamba ni fursa nzuri ya kufanya kazi kama mjakazi
Hata hivyo alipowasili, aliyepaswa kuwa mwajiri wake alimkataa kwa kukosa kitambulisho cha kitaifa hivyo kumsababisha Mbithe kukwama asijue la kufanya
Alimwomba dereva wa lori ampe lifti ya kurejea nyumbani ila baadaye dereva huyo alimtupa nje baada ya Mbithe kukataa kutongozwa naye
Baada ya kushuka kutoka kwa lori hilo, alishambuliwa na fisi na kuachwa bila mkono, jicho pamoja na majeraha mengine
Mwanamke ambaye ni mwenyeji wa Machakos na aliyeshambuliwa na fisi katika Mbunga ya Wanyama ya Tsavo baada ya kufukuzwa na madereva wa Lori kwa kukataa kutongozwa nao, anatafuta haki.


Hadithi ya Irene Mbithe mwenye umri wa miaka 23 ilianza mnamo Agosti 20 mwaka wa 2018, alipokuwa akisafiri hadi Mombasa kufanya kazi ya nyumba.

Kulingana na shirika la Usikimye, linalowasaidia waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia, mwanamke huyo alipigwa na butwaa baada ya aliyepaswa kuwa mwajiri wake kumkataa kwa kukosa kitambulisho cha kitaifa.




 
Mbithe alikosa nauli ya kurejea nyumbani ndipo akaomba lifti kutoka kwa dereva wa lori.

Dereva huyo wa lori alianza kumwandama ila alikataa, na kutolewa kwenye lori na kubwagwa kwenye mbuga ya wanyama ya Tsavo," shirika la Usikimye lilisema.

Alipokuwa ameketi kando ya barabara, Mbithe alivamiwa na fisi na kupoteza jicho, mkono na kuachwa akiuguza majeraha mabaya. Msamaria mwema alisikia Mbithe akipiga kamsa na kuwaita polisi na maafisa wa Huduma kwa Wanyama Pori, (KWS) waliopata akiburutwa na fisi huyo hadi barabarani hata wakadhania mwanamke huyo alikuwa amekuwa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post