Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameshangazwa Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha tani 138,262 kwenda Uganda wakati nchi hiyo inatumia bandari nyingine kusafirisha mamilioni ya tani.
Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 27, 2021 jijini Dar es Salaam saa chache baada ya kumpokea Museveni ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.
"Kwa hiyo tumekubalia hapa kuongeza mzigo unaotoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Uganda. Pia nimemuomba Museveni aridhie kupitisha shehena ya mizigo na vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa bomba la mafuta kupitia Bandari yetu ya Dar es Salaam nadhani hilo litafanyika.
"Kwenye la Bandari pia tumemuomba Museveni aruhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wakafungue ofisi Kampala ili kurahisisha utendani na ufanyaji kazi wa bandari kwa wafanyabiashara wa Uganda, nalo amelipokea kwa mikono miwili na amekubali," amesema Samia.
Post a Comment