Mke Amfanyia ‘Kitu Mbaya’ Staa wa Soka"





MPACHIKAJI mabao wa zamani wa Orlando Pirates, Tendai Ndoro, amejikuta akipoteza mali zote alizochuma baada ya kukorofishana na mkewe aitwaye Thando Maseko.
Katika kilele cha penzi lao, Ndoro aliyewahi pia kung’ara akiwa na timu ya taifa ya Zimbabwe, aliandikisha jina la bibiye huyo kwenye mali zote, yakiwamo magari na nyumba.

Sasa, kilichotokea ni kwamba wawili hao wametibuana na alichokifanya bi. Thando ni kumfukuza mshikaji kwenye mjengo waliokuwa wakiishi, ikizingatiwa kuwa ndiye jina lake linalotumika kwenye umiliki.

 Download Our Udaku Special APP Kutoka Google Play Store Kwa Kutumia Link Hii Hapa>>>


Taarifa za Ndoro ‘kufulia’ zilianza kusambaa nchini Afrika Kusini hivi karibuni baada ya mwanasoka huyo kuonekana akiwa amepungua uzito, ambapo ilielezwa kuwa huenda anasumbuliwa na tatizo la akili.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post