Nge waliosambaa kusini mwa Misri wamewauma watu watatu hadi kufa baada ya dhoruba kali kuwakimbizika katika makazi yao na kuwaleta mitaani na majumbani.
Takriban watu 450 zaidi walijeruhiwa kwa kuumwa na nge hao, afisa wa wizara ya afya alisema.
Mji wa Aswan kusini mwa Misri ndio ulioathirika zaidi na uvamizi wa nge hao, ambapo mvua kubwa ya mawe pamoja na radi katika eneo karibu na Mto Nile ilishuhudiwa siku ya Ijumaa.
Kawaida mvua kubwa ikinyesha nge husombwa kutoka kweye maficho yao na kuzagaa mtaani kama ilivyo kwa nyoka, ambao pia husombwa na maji kutoka kwenye mashimo yao.
Mamlaka nchini humo zimechukua hatua ambapo mpaka sasa dozi za ziada za kuzuia sumu zimetolewa kwa vituo vya matibabu katika vijiji vilivyo karibu na milima na jangwa, afisa wa afya aliliambia shirika la habari la Al-Ahram.
Madaktari waliokuwa wanaendelea na shughuli za kutoa chanjo sasa wamelaziika kuelekeza nguvu kutibu watu walioumwa na nge, afisa huyo aliongeza.
Watu wamehimizwa kupunguza kutembea mitaani na kukaa kwa tahadhari majumbani pamoja na kuepuka maeneo yenye miti mingi.
Marufuku ya kusafiri
Gavana wa Aswan, Ashraf Attia, ametangaza masharti ya watu kusafiri katika mji huo kutokana na hali ya hewa ya mvua kubwa na ukungu unaosababisha madereva kutoona vizuri.
Video mbali zimewekwa kwenye mitandaoni ikiwemo mtandao wa pulse kuonyesha namna mvuo ilivyo kubwa katika mji huo.
Sumu ya nge
Nge wana miguu minane, na hutambulika kwa urahisi kwa namna walivyo kichwani kama mfano wa siafu kidogo na mkia wake wenye sumu na uliogawanyika, Wanaishi hasa katika jangwa lakini wamezoea
Hali mbalimbali za mazingira, na wanaweza kupatikana katika mabara yote isipokuwa Antaktika.
Kuna zaidi ya aina 2,500 zilizoelezewa za nge na familia 22 zilizopo (hai) zinazotambuliwa hadi sasa. Watalaam wanathibitisha kuwa nge ana sumu ambayo ni mchanganyiko unaojumuisha 'neurotoxins'
ambayo huathiri mfumo wa neva wa mtu aliyengatwa (mwathirika). Kuumwa na aina fulani ya nge hatari kunaweza kusababisha kupooza, degedege kali, matatizo ya moyo, matatizo ya kupumua na hata kifo.
Post a Comment