Kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii, mnamo Jumamosi Novemba 27, Natasha aliashiria kwamba amempata mwanamume anayemfaa. Alimtambulisha nabii wa kihindi na kupakia picha kadhaa akiwa na nabii huyo aliyetambulika kama Carmel.
Wawili hao walivalia mavazi meupe ya kufanana ya jamii ya Wahindi, yanayojulikana kama sarees, huku picha nyingine ikimuonyesha Natasha akitengeneza vazi la nabii huyo huku wakitupiana tabasamu la kuyeyesha mioyo.
Natasha aliwajulisha wafuasi wake kimafumbo kwamba ameshapata ubavu wake.
“Mungu amekifanya kila kitu kiwe kizuri kwa wakati wake,” alisema huku akitoa fungu la Biblia kutoka kitabu cha Mhubiri 3:11.
Mwanafunzi Mwenye Umri wa Miaka 14 Aliyetoweka kwa Wiki Moja Apatikana
Picha zingine alizopakia zilionyesha Natasha akiwasili katika kanisa lake la Nairobi akiwa ameshikana mkono na nabii huyo, dhihirisho kwamba wana uhusiano wa kimapenzi na wala sio wa mahubiri pekee.
Wawili hao walikaribishwa katika Kanisa la Empowerment Christian lililoko Nairobi na mashemazi waliovalia mavazi vizuri ya kuvutia. Carmel alitembea sako kwa bako na Natasha akiwa amebeba maua ya kupendeza. Hatimaye walihubiri wakati wa ibada kwenye kanisa hilo.
Post a Comment