Matumaini Ya Tanzania Kufuzu Kombe La Dunia 2022 Yazimika





TAIFA Stars jana imetibua matumaini yake ya kufuzu Kombe la Dunia 2022, baada ya kuchapwa na DR Congo mabao 3-0 nyumbani, kwa Mkapa.


Stars imepokea kipigo hicho licha ya kuwa na hamasa kubwa kabla ya mchezo, pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhudhuria mchezo huo jana.



Taifa Stars sasa imebaki na pointi saba katika msimamo wa Kundi J na kama Benin ilishinda dhidi ya Madagascar jana usiku, itakuwa imekwea kileleni huku kila timu ikiwa imebakiza mchezo mmoja kabla ya kumaliza hatua ya makundi.

 

Sasa mchuano halisi wa timu itakayomaliza kileleni umekuwa ni Stars, DR Congo na Benin.


Matumaini halisi ya Stars ilikuwa ni kuiombea Benin nayo ifungwe jana usiku, lakini kama ilishinda basi safari ya Stars kuelekea Kombe la Dunia imebaki kwa asilimia chache sana.


Matokeo hayo yaliifanya Congo isonge hadi nafasi ya kwanza ikiwa na pointi nane kabla ya mchezo
wa Benin (pointi 7) na Madagascar (pointi 3) jana usiku.

 


Stars itacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Madagascar keshokutwa Jumapili ugenini na inatakiwa ishinde tu ili angalau kuwa na matumaini kidogo yaliyobakia.

 

Katika mchezo wa jana, DR Congo walipata mabao yao kupitia kwa Kakuta Mambega kipindi cha kwanza na Idumba Fasika dk ya 66. Dk 86 Malango Ngeta aliifungia Congo bao la tatu.

Stori na Wilbert Molandi





0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post