Maskini Zamaradi Afunguka Kwa Uchungu Jinsi Mama yake Alivyofariki Mikononi Mwake


Ameandika Zamaradi Mketema :

"28-11-2012 Ndio siku uliyonifia mikononi, tena ikiwa kipindi kifupi baada ya BABA nae kufariki, Na mpaka leo hii ni miaka 9 kamili tangu uondoke kwenye uso wa hii Dunia, ilikuwa ni asubuhi kama hivi, siku niliyoamka na uvivu wa ajabu ambao sikupata kuwa nao kabla, na nadhani ni kutokana na hekaheka za usiku wake tuliokupeleka hospitali, usiku ulionitamkia umechoka sana, kwa mara ya kwanza nilikwambia shahadia, sielewi ujasiri nilitoa wapi, na ulifanya mara nyingi kama wimbo!! task yangu kubwa kwa asubuhi hiyo kabla ya kufika ilikuwa ni kwenda hospitali uliyokuwa kabla kuchukua rekodi yako kwa ajili ya ulikokuwepo, nikiwa njiani naelekea napigiwa simu nirudi kwanza, nageuza nafika nakuta umezidiwa tena!! Oxygen iliyowekwa haikusaidia chochote, nikiwa nimesimama pembeni yako nikanotice hapo shingoni panapiga katika speed kali isiyoeleweka, kadri muda ulivyokuwa ukienda speed ikawa inapungua na kupungua huku naishuhudia, na mpaka ikawa taratibu kabisa na hatimae ikazima, sikuwa Daktari lakini nilijua umeaga, natoka nje mbio nawaambia wasaidizi kwa hofu kubwa njoo Mamaangu amekufa, tunaingia wananiambia ungetoka kidogo, natoka lakini nashindwa narudi bila ruhusa, nakuta wanakufunika shuka hadi kichwani, nikasema Basi!! Nguvu ziliisha, nilikuwa natembea sioni mbele, pochi naiburuza chini, ninachokumbuka niliisahau gari yangu palepale hospitali na kuingia kwenye Tax, Mpaka tunafika Salenda Bridge Tax ndio ananiuliza samahani Dada kwani tunaelekea wapi!!? Ndio nakumbuka na kumuelekeza, ilikuwa siku NZITO sana ya maisha yangu!!! Kama ni UIMARA wa maisha niliyokuwa nao niliupata kuanzia kwako, nimekuuguza kwa muda mrefu sana MAMA, ilifikia kipindi mgonjwa anakuangalia anatoa machozi, unamuuliza Mama nini hajibu kitu anasmile tu!! Mara nyingine hali unayokuwa nayo natoka nje Naliaaa, kisha nafuta machozi narudi ndani najichekesha na kujifanya kilakitu kiko sawa, bado nakumbuka kauli yako, ”Mwanangu nakuonea huruma, umechoka sana!” Kikubwa namshukuru sana MUNGU kwa kunipa nafasi ya Kukuuguza na kukuhangaikia mwanzo mpk mwisho,kama BARAKA ZA MZAZI nimezipata kwa hali ya juu, na namshukukuru MUNGU sana.

Bado nakukumbuka sana MAMA,
Ulale Salama,
na asante kwa kilakitu 🌹🕯


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post