Rapa French Montana Atangaza Kuachia Album Yake Mpya “THEY GOT AMNESIA” Ambayo Ni Ya 4 Na Itatoka Novemba 12 Mwaka Huu
Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram Amethibitisha Hilo Kwa Kuandika Ujumbe Wa Historia Yake Miaka 2 Iliyopita Akisema
✍“(THEY GOT AMNESIA) Albamu novemba 12. Niko na furaha kuwapa story yangu. Miaka miwili iliyopita siku kama hii nilikuwa ICU(Chumba cha mahututi) kupigania maisha yangu. Nilipoteza kumbukumbu zote, nilipoteza marafiki, nilipoteza matumaini, nilipoteza karibu kila kitu. Na mwishoni kabisa nikagundua sina vyote ila nimebaki ni Mungu tu alie mkuu. Akanishika mkono, akanipa matumaini tena. Wakati najaribu kurudi kwenye game, walinihesabu kuwa nimeisha kabisa, na wakasahau kila kitu tulichokifanya pamoja. Siku ya 730 sasa, “THEY GOT AMNESIA” albamu Itatoka Novemba 12” -French Montana
Post a Comment