Mashabiki wa Alikiba wanatia huruma..Msijindanganye Diamond Platnumz yupo Levo Zingine


Mashabiki wa Alikiba wanatia huruma sana, Wengi hawawezi kufikiri mbali ya kile wanachokiamini kuwa “Alikiba ni msanii mkubwa na anasauti nzuri alishawahi kuimba na R Kelly”.

Hua hawaoni zuri lolote la Diamond bali mabaya tu na hua hawaoni baya lolote la Alikiba, ukiwauliza sababu ya kumchukia Mondi utasikia eti anaimba matusi, nyimbo zake anakopi, haimbi za kuelimisha n.k n.k.

Ukiwaambia huyo asiyekopi wala kuimba matusi mbona hamshindi wanasema eti D ni freemason, anatungiwa nyimbo na freemason wengine huenda mbali zaidi na kusema kua Mond huwa anafanya ********* ndio maana anaendelea kua maarufu. Ukiwauliza kwani Diamond ndio msanii freemason pekee, wanasema yeye anacheo kikubwa kuliko, Inshort hawana Strong Point.

Mashabiki wa Alikiba ndio wanaongoza kutukana mitandaoni, acheni kuwa mashabiki lialia au mashabiki maandazi, kuweni positive, fungueni bongo zenu muwe mnawaza nje box msikariri kitu kimoja kama Computer inavyojua 0 na 1 pekee.

Mnajiabisha na kumuaibisha mnaemshabikia mnazidi kutuaminisha kua Anashabikiwa na watu wasiothamini Mchango wa wasanii wengine.

Binafsi hainiingii akilini kua kipindi ulipokua mtoto ulikua na kiburi, mama yako unamtukana, ugomvi, matusi hayakauki mdomoni hadi mama yako akanyoosha mikono na kuacha dunia ikufunze harafu leo uje usubirie Alikiba aimbe akufundishe tabia kwa kuimba vitu vya adabu, Kama ulishindikana kwa mama yako usitegemee kunyooshwa tabia na Diamond au Alikiba kwa kisingizio eti wao ni kioo cha jamaii.

Wasanii wote wapo ajili ya kutafuta pesa waendeshe familia zao hata huyo Alikiba mnaona anaheshima haimbii kwa ajili ya kutaka pesa ni kwakua kashindwa kuugeuza mziki wake ukampatia pesa anazozihitaji. Alikiba anazihitaji sana pesa kutoka kwenye muziki basi tu anashindwa afanyeje ili aweze kuzipata maana hajui biashara wala kuhendo mashabiki wake. Siku akijishusha akaenda kwa Diamond kupigwa msasa jinsi ya kupiga pesa kwa muziki, kwa kipaji kile alichonacho atapiga hela sana. Kiburi kinamponza anakufa kwa kinyongo na chuki.

Guys amkeni, acheni kuwa negative kwa kila kitu.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post