Mama Mwenye Nyumba Achoma Nyumba yake Kisa Wapangaji Kuchelewesha Kulipa Kodi


Mama mwenye nyumba jina Caroline Mukolwe wa eneo la Mumias, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya ameichoma nyumba yake moto kutokana na Wapangaji wake kutolipa kodi kwa wakati .

Taarifa ya DCI inasema Mama huyo alimtaka Mpangaji wake Teresia Ayeng alipe kiasi cha kodi anachomdai juzi Alhamisi ambacho ni Ksh. 800 sawa na Tsh 16,494 lakini Teresia akalipa Ksh. 400 sawa na Tsh. 8,247 kupunguza deni huku akiahidi atalipa nyingine baadaye.

Mama mwenye nyumba alipoona fedha ya kodi anayodai haijalipwa yote akarudi kwenye nyumba yake na kubeba mafuta ya taa akamwagia ndani ya nyumba kisha akaifunga na kuipiga kibiriti, Mpangaji akashuhudia mali zake zote zikiteketea kwa moto"

Kwa sasa Mama mwenye nyumba huyo anashikiliwa na Polisi kwa kumsababishia hasara Mpangaji wake ya kuchoma mali zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Ksh. 47,000 sawa na Tsh. Laki 9.69.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post