MSANII wa kike wa Bongo Fleva, Careen Gardner almaarufu Malkia Karen anasema kuwa, anawashangaa mno watu wanaompangia mtoto wake baba, jambo ambalo linamuumiza kwani kama ni mtoto amezaa yeye mwenyewe.
Akizungumza na Gazeti la Ijumaa juu ya ishu hiyo, Malkia Karen ambaye ni mtoto wa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Gardner G Habbash anasema kuwa, anaumia mno kila kukicha kutokana na mtoto wake aliyejifungua hivi karibuni kupewa baba wakati ukweli anaujua yeye mwenyewe.
“Jamani tangu nikiwa mjamzito baba wa mtoto mnanipa ninyi? Mtu anakupangia mtoto, kweli ni sahihi hiyo? Mimi ni mama na mimi najua wazi baba wa mtoto ni nani hivyo wasinipangie kabisa, wanakosea sana.
“Mtoto wangu ipo siku atakuwa na kuona hayo, sidhani kama atapenda kwa kweli,” anasema Malkia Karen ambaye baba wa mtoto wake amekuwa akihusishwa na mastaa kama Diamond Platnumz na Rayvanny.
Lakini Gazeti la IJUMAA linafahamu kwamba mtoto huyo siyo wa mastaa wanaotajwa bali ni wa jamaa ambaye siyo staa na ni mfanyakazi wa serikalini asiyependa mambo ya mitandaoni kutokana na aina ya kazi yake.
STORI; IMELDA MTEMA
Post a Comment