Makubwa...Fisi Atafuna Kiganja Cha Mkono

 


Emmanuel Ndete (20), mkazi wa Kata ya Kharumwa, wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa mpaka kukatwa kiganja cha mkono na Fisi, usiku wa Oktoba 29  majira ya saa 2:00 usiku wakati anarudi nyumbani kwake.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Geita Dokta Hiporitas Msimbe, amesema walimpokea mgonjwa huyo Oktoba 30, 2021, akitokea hospital ya wilaya ya Nyang’hwale akiwa  katika hali mbaya na kumpatia matibabu ambapo baada ya matibabu ya awali alipatiwa rufaa ya kwenda hospitali ya Bugando.

Itakumbukwa kuwa miezi saba iliyopita kikosi cha waganga wa jadi kutoka mkoani Shinyanga kilifanya operesheni maalum kwa ajili ya kumaliza Fisi hao ambapo walifanikiwa kuuwa Fisi zaidi ya 58 ambao walikuwa wakivamia na kupoteza maisha ya watoto kwa wakubwa na kupelekea watu kuishi kwa wasiwasi.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post