Kundi la P Square Waamua Kuweka Tofauti zao Pembeni



Taja makundi yote kwenye muziki Afrika lakini usisahau kuwataja Psquare katika orodha yako .

Baada ya kipindi cha muda mrefu kundi lao kuvunjika na kila mmoja kubaki solo artist Psquare ( Peter and Paul ) wameamua kuweka tofauti zao pembeni na sasa kila mmojaa amemfollow mwenzake instagram .

Hii imekuja baada ya Anitha Okoye Dada yao kupost Video kwenye ukurasa wake wa Instagram Peter akiwa na watoto wa Paul ambaye ni kaka yake akiwa amewapeleka shopping .

Kundi hili limevunjika tangu 2016 Vyanzo vikitajwa ni vingi ( ikiwemo ya Dada yao Anitha okoye kutaka kumsimamia Paul )

lakini mbali na hayo ni mvurugano uliotokea baina ya Peter and Paul na Kaka yao Jude Okoye, Peter alitaka Kaka yake Aachie ngazi asiwe manager ili asije kumvunjia heshima lakini Kaka akamtishia Dogo ikabidi Dogo atulie .


Wakiwa wanasafiri pamoja kwenye Private Jet mambo yaliendelea na wote hawakuzungumza mpaka wanafika na kila mmoja kuchukua hamsini zake kumbuka hapo Peter hajaongea na Paul toka 2015 .

Kupitia twitter the Next day Kaka mtu akaandika kwamba sio manager wa Kundi hilo na Chochote kitakachotokea ni Juu yao hausiki .

Tatizo likaendelea walikuwa tayari mbioni kuachia album yao Double trouble na baadhi ya ngoma walikuwa wameshirikishwa unaambiwa kuna baadhi ya ngoma zikatoka Peter hayupo kwenye Video .

Sasa moja kwa moja Peter akamind akaona kama Paul anataka kumgombanisha na Wasanii aonekane yeye hatokei kwa video, wakiwa Marvin Records Tifu tifu likatokea baadae Peter akamwambia Paul next time Utakuwa mwenyewe kwa video lakini video iliyofuata ilikuwa na Mr Flavour na Mr flavour alimbembeleza sana paul hadi kaongea Ki Igbo ndio mchizi akakubali lakini alijua kuna video nyingine itakuja tu hatotokea .

Kwa kufupisha tu Mambo yaliendelea mpaka kufika kuwa makubwa majamaa kutaka kuzichapa mambo yakawa mengi kila mtu akachukua hamsini zake baadae wakarudi kurekodi ngoma mbili tatu ikiwemo ya Mondi wakiwa wameshirikishwa na walikuja kushoot video kila mtu kivyake kwa Heshima ya Mondi baada ya hapo tena Tofauti zikarudi upya 😊😊 .

Naam kwa Ishara hii iliyotokea huenda tukategemea Peter and Paul Kurejea kama Psquare !!? .



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post