Kumekucha..Nikki Mbishi Amchana Vibaya Ali Kiba "Ali Kiba Ukitoa Chorus Kwenye Nyimbo zake Vingine Anaunga Unga tu Melodies Hakuna Kitu ni Vumbi tu"




Rapa tokea kikosi kazi, Nikki Mbishi kupitia ukurasa wake wa twitter amemvaa @officialalikiba kuwa ukitoa chorus, vingine anavyo fanya kwenye nyimbo zake ni ujanja ujanja tu na vimelody vya kuunga unga. Akiitolea mfano wimbo wa Mvumo wa radi.




“Ali Kiba ukitoa choruses zake kwenye verse huwa anaunga unga sana,vijimelody 'flan' ujanja ujanja tu halafu basi ndio #KING na Jiji linasimama

Sio kama hakuna alizootea hapana ila "Mvumo wa Radi" ni ile chorus,bridge na beat basi vingine VUMBI tu!
Bongo bwana!”

HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL APP, DOWNLOAD HAPA UWE NAYO KWA SIMU YAKO..USIPITWE


Nikki amekuwa ni moja ya wale wasanii wakongwe na walalamikaji hasa wakiamini hii sanaa inapewa kipaumbele kwa watu wasiojua na wao wenye kujua wakipewa kisogo. Nikki aliwahi hadi kuwadis wanae wa kundi moja akiwemo P Mawenge,amedis media kibao na sasa kahamia kwa waimba Bongo Flava




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post