Jamaa Aliyetaka Kumuua Rapa Eminem Mwaka 2020 Akutwa na Hatia Nyingine



Kijana anayefahamika kama Mathew David Hughes aliyetaka kumuua Rapa Eminem kwa majaribio kadhaa mwaka 2020 aingia tena matatizo baada ya kumvamia mlinzi wa Mall huko Marekani .

Hughes akiwa na miaka 28 tu alikutwa na hatia kwa makosa ya uvamizi na uharibifu wa mali na baada ya mashtaka ya kwanza kufutwa alikutwa na hatia tena ya uvamizi kwenye nyumba ya Rapa Eminem .

Mbali na hayo Hughes ambaye alikuwa anatumukua kifungo cha nje amekutwa na hatia ya kutohudhuria Kesi yake mahakamani na kosa lingine ni kumvamia Mlinzi wa Shopping Mall .

Hughes baada ya kumvamia Eminem nyumbani kwake alihukumiwa miaka 5 na alitumikia siku 524 na baadae kupata msamaha kutumikia kifungo cha nje huku akiwa chini ya uangalizi na sasa imetajwa hukumu yake itatolewa Disemba 15 .



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post