Hatimaye Kanye West na Drake Wapatana


Moja ya jambo ambalo lililokuwa linasubiriwa na wapenzi wengi wa burudani ni kuona marapa kutoka Marekani, Drake na Kanye West 'Ye' wamelizika bifu lao, na hatimaye hilo limetimia.

Wakali hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitupiana maneno, wameonekana wakiwa pamoja usiku wa kuamkia leo.

Katika kuthibitisha hilo, mtu wa karibu na rappa Kanye West, 'Jason' alitumia ukurasa wake wa twitter kunyoosha maelezo juu ya video hiyo. 

"Drake Squashed The Beef With Kanye West Last Night In Toronto " - Jason.

Itakumbukwa, mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia video aliyoipost rappa Kanye West 'Ye' kwenye ukurasa wake wa instagram, alimuomba Drake waimalize bifu yao na wafanye tamasha la pamoja mwishoni mwa mwaka huu kwa ajili ya kupaza sauti zao kwa lengo la kumsaidia #LarryHoover kutoka gerezani.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post