Dudu Baya "Nilimvunja Mr Nice Kiuno Baada ya Kuniletea Dharau"

Kwenye muda ambao hakuna mitandao ya kijamii,Bongo Flava ilikuwa na msanii mkubwa na aliyekaa juu kimafanikio akijizolea umaarufu nchini, Afrika Mashariki na Kati, akipiga mashow ya hatari nchi nyingi za Afrika na hata nje ya bara, Hii yote ilitokana na aina ya muziki wake uliyokuwa na maudhui kama ya watoto hivi na akaupa jina TAKEU (Tanzania,Kenya, Uganda),namzungumzia Lucas Mkenda maarufu kama MR. NICE.

Mr. Nice alijikuta akiingia kwenye mgogoro na msanii Dudu Baya, japo haikujulikana hasa chanzo ni nini, ila kuna watu walidai tofauti zao zilianza baada ya kuanza kugombania upambe kwa tajiri mmoja tokea Morogoro aliyejulikana kwa jina la Merey Balhabou, kama ilivyokuwa jadi kwa mapedeshee wengine nchini mfano Jack Pemba,pedeshee Musofe Ndama Mutoto ya Ng'ombe na wengineo kuwa na wapambe.

Bifu lao lilipelekea hadi Mr. Nice kuvunjwa kiuno na Dudu Baya akiswekwa Rumande. Baada ya miaka mingi kupita,2019 Dudu Baya alifunguka sababu kubwa zilizofanya ampige Mr. Nice,akidai alimletea dharau walipokutana klabu hivyo akaamua kumfunza adabu.

Wawili hawa walizika tofauti zao na hadi sasa kila mtu anaishi maisha yake.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post