Staa wa muziki barani Afrika kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amesema anaendelea kuwekeza katika biashara mbalimbali ili ikitokea hata asipofanya muziki, bado maisha yake yaendelee kama kawaida.
Diamond amefunguka hayo katika mahojiano na BBC alipoulizwa ni athari zipi zilizokumba muziki wakati wa mlipoko wa UVIKO-19 na alikabiliana nazo vipi.
“Nimekuwa katika mazingira ambayo naiogopa sana kesho, nilikuwa nasema kesho na keshokutwa ikatokea siwezi kuimba nitawezaje ku-maintain mapato yangu, so nimewekeza kwenye vitu mbalimbali ambapo hata leo nisipoimba muziki nitaishi maisha haya na ninaweza kuendeleza kupata pesa.
“Kwa ujumla katika tasnia imetufunza vijana wengi lazima tuwekeze, huu muziki au kiwango cha pesa tunachokipata katika muziki, tumia hii kama njia chanya ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali ili kesho na keshokutwa hata tusipoweza kufanya show tuweza kutengenza riziki kwa nama nyingine,” anasema Diamond.
Diamond ameendelea kusema; “Mimi nimekuwa katika mazingira ya kuheshimu sana digital, naamini imewaamsha na watu wengine kuwekeza katika digital kwa sababu wakati ule ulikuwa huwezi kukutana na mtu, unaweza kutumia digital kujipatia mapato.”
Ikumbukwe Aprili, 2020, Diamond alisema alikuwa amepata hasara ya shilingi bilioni 3.5 kutokana na kuhairishwa kwa shoo zake alizotarajia kuzifanya katika nchi zaidi ya 10 kufuatia mlipuko wa UVIKO-19 duniani kote.
CC; @sifaelpaul
Post a Comment