Davido Kikaangoni, Akosa Tuzo Miaka Mitatu, Wadau Wamshauri Afukuze Meneja



Ule msemo wa mvumilivu hula mbivu umewashinda mashabiki wa Davido wanaoweza ni wa Manchester United 😄 .
Kupitia Twitter Moja kati ya Shabiki wa Msanii huyo kutoka Nigeria ameamua kumchana na kumwambia kama anahitaji afike mbali kwenye muziki inabidi achukue hatua ya kuachana na meneja wake Asa Asike .

Sababu kubwa Shabiki anasema Meneja huyo sio mbombevu wa kulifahamu soko la muziki nchini Marekani so itamfanya ashindwe kufanya vizuri ikiwemo kuchaguliwa kuwania hata tuzo za Kimataifa .

Shabiki kaongea ya moyoni unaambiwa anasema Hata Burna Boy aliamua kumpumzisha Mama yake kutokuwa meneja wake pale umaarufu ulipoongezeka hivo hivyo kwa wizkid ambaye aliamua kuachana na meneja wake Sunday na hawakuachana kiugomvi ila aliwapumzisha yote ni ili afike mbali kimuziki .

Shabiki amedai kuwa hakuna msanii Nigeria ambaye ametoa hit song nyingi kuliko yeye ndani ya miaka 3 lakini hakuna cja ajabu kinachoendelea .

Ameenda mbali zaidi na kumwambia Davido anachotakiwa kufanya ni kutafuta meneja ambaye analijua soko la muziki Marekani ambaye akipiga simu kwa wakuu wa media houses Marekani wana respond Chap tu' .

Kwa mujibu wa shabiki anasema Davido kama ni kushinda local Awards basi hazizidi tuzo 5, Amemtolea mfano wizkid ambaye alitoa Wimbo Wake JORO uliobeba tuzo kibao mwaka ambao yeye ameachia Album. .



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post