Bifu Kwishney Shilole Adai Kumkubali Ali Kiba "Sina Kinyongo nae"



Kwa mujibu wa dada wa taifa, @mangekimambi_ amechati na @officialshilole amefunguka kumkubali @officialalikiba na akidai kwenye interview aliyofanya kwenye Refresh kuhusu followers hakudhamiria kumdharau kabisa Alikiba na hakuwa serious kwenye hilo.

Kwenye post hiyo ya Mange a.k.a Mandy, Shilole amecomment kuwa yuko vizuri kwasasa na hawekagi vitu moyoni. Kingine Shilole amedai kutokuwa na tatizo lolote na mjasiriamali mwenzie @esha.s.buheti na wako vizuri kabisa tena wamezidi kuwa vizuri zaidi baada ya hizi purukishani za siku mbili tatu za hivi karibuni.

Ikumbukwe sakata hili lilianza Alhamis ya tarehe 28/10 Alikiba alipokuwa kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm na kudai hakumualika Shilole kwenye Listening party ya albamu yake (ONLY ONE KING) iliyofanyika October 6, Serena Hotel jambo ambalo lilimkwaza Shishi kuchoreka kama mvamizi kwenye shughuli za watu😂 na kuamua kujibu tuhuma hizo kwenye kipindi cha Mashamsham ya Wasafi FM huku akimuua vibaya King Kiba.

Hasa itakuwaje kwa Snura aliyetunga na wimbo?😁




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post