Akaunti ya Benki ya Mwanafunzi wa Chuo Yakutwa na Bilioni 2.3, Serikali Yashtuka



Mahakama ya kupinga rushwa nchini Kenya imetoa amri ya benki kuzuia akaunti ya mwanafunzi Felesta Njoroge, ambaye ana umri wa miaka 21, hiyo ni baada ya kukutwa na salio la Sh bilioni 2.3.

Mamlaka ya Asset Recovery Agency (ARA) imezuia akaunti hiyo baada ya kugundua kuna wingi wa fedha katika akaunti hiyo wakati mhusika ni mwanafunzi.

Njoroge alipoulizwa juu ya fedha hizo ameeleza kuwa alitumiwa na mpenzi wake wa Ubelgiji, Marc De Mesel na kuambiwa kuwa anaweza kutumia kadiri anavyotaka.

Mamlaka imeagiza kuwa fedha hizo zizuiwe kwa muda wa siku 90 ili uchunguzi ufanyike.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post