Afya ya Rais Biden iko sawa baada ya kufanyiwa uchunguzi




Afya ya rais wa Marekani Joe Biden imeelezwa kuwa nzuri baada ya hapo jana kiongozi huyo kufanyiwa uchunguzi wa kina na wa kawaida na kulazimika kukabidhi kwa muda mamlaka yake kwa makamu wa rais Kamala Harris. 


Daktari wa Ikulu ya White House Kevin O'Connor amesema katika ripoti yake kwamba rais Biden yuko imara kuendelea na majukumu yake kikamilifu kama mtendaji mkuu, mkuu wa nchi na Amiri jeshi Mkuu.




Biden ambaye leo anatimiza umri wa miaka 79, ndiye rais mwenye umri mkubwa katika historia ya Marekani. 



Wakati wa uchunguzi huo wa kimatibabu, Biden alilazimika kumkabidhi madaraka Harris ya ukuu wa nchi. Kwa muda wa saa moja na dakika 25, Harris alikuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa rais wa Marekani.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post