Zaidi ya watu 40 wafariki ajali ya moto




Zaidi ya watu 40 wafariki ajali ya moto
Watu wasiopungua 46 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuwaka kwenye jengo moja lililopo Kusini kwa Taiwan leo Oktoba 14, 2021.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNA la China, moto huo ulianza asubuhi katika jengo la biashara la ghorofa 13 Wilaya ya Yancheng, ambapo zaidi ya maafisa wa ukoaji 337 wanaendelea na shughuli za uokoaji.

Msemaji wa kikosi cha zima moto mji wa Kaohsiung aliambia CNN kuwa zaidi ya watu 41 wamejeruhiwa na kuonya kuwa huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka zaidi kutokana na baadhi yao kunasa kwenye jengo.

Taarifa za awali, haijafahamika chanzo cha moto huo, ambapo kwa mujibu wa CNA   polisi wameanza uchunguzi kwa kupitia baadhi ya mikanda ya video



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post