Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amewaomba wasomi wote wenye shahada waliopo mkoani humo, kufika ofisini kwake awasaidie kupata mafunzo na mitaji, ili wajiajiri katika sekta mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa samaki wa vizimba.
RC Gabriel amesema kuwa vijana wote wenye elimu ya juu kupitia mpango maalum atawasaidia kupata mafunzo ya ujasiriamali, mitaji na masoko kwa ajili ya bidhaa watakazozalisha.
Mhandisi Gabriel, amesisitiza kuwa mkoa wa Mwanza una vijana wengi wasomi lakini lakini hawana kazi za kuwaingizia kipato na yeye amejitoa kuwa mwalimu na kuwapa njia za kufanya ili waweze kujipatia kipato.
Post a Comment