KOSA SIO LA MTU MMOJA!
Muziki wa TZ haujaharibiwa na Mtu au Kitu kimoja! Kila mshika mdau (Shakeholder) katika ngazi zote za mnyororo wa uzalishaji, ame-play part...
Na pia, kuna baadhi ya circumstances zimetokea na kuuathiri pasipo kusababishwa na washika dau wakuu.
Sio sahihi kumsingizia mtu mmoja! Alilaumiwa Ruge Mutahaba kama ndio mchawi, ameondoka ila bado tuna hali ile ile kama sio mbaya zaidi. Inaonyesha pia kuna Kundi linamtupia msanii mmoja (Diamond) lawama pia, ila nayo sio sahihi!
Na mimi navyoandika maandiko yanayohusu Sanaa, huwa simlengi mtu mmoja bali naongelea kiujumla. Nikiamua kumsema mtu sishindwi kumtaja directly!!!
Hivyo basi, kama ambavyo nasisitiza kuwa kuiinua Tasnia itahitaji Collective Effect (nguvu ya pamoja), basi jua kuwa kilichoiangusha pia kilikuwa jitihada za pamoja. Wapo ambao wamezingua zaidi ya wengine ila kama nilivyosema jana HATUCHEKANI... na risiti za ushahidi ZIPO!! But lets heal...
Angalizo: Usisome ili ujibu, some ili uelewe.
The Leader! Wakazi
Post a Comment