Wadau Wanauliza Hivi Paula Anasoma Muda Gani?




Paula Kajala; mtoto wa mwigizaji Kajala Masanja anaendelea kuibua gumzo akiwa chuoni huko nchini Uturuki, lakini kuna swali linaloulizwa na wengi; kwamba anasoma muda gani?

Kwa nini? Hii ni kwa sababu haupiti muda bila kuposti picha au video zikimuonesha akiponda raha kwenye migahawa mikubwa nchini humo.

Picha na video hizo anazoposti mara kwa mara kwenye Insta Story yake ni pamoja na picha za mpenzi wake Rayvanny na kujaribu kueleza jinsi anavyompenda.

Kwenye video, nyingi ni zile zinazomuonesha akiimba nyimbo za kimahaba za Rayvanny akimkumbusha jamaa huyo kwamba anampenda na amemmisi.

Pamoja na kwamba kuna swali lingine la ni nani anayempa bata kwenye migahawa na hoteli anazojiachia, ishu kubwa ni muda gani anautumia kusoma kwa sababu hakuna picha wala video ambazo ameposti zikimuonesha labda akiwa darasani au maktaba akijisomea!

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba, Paula anapenda mno mambo ya fasheni ndiyo maana anapiga picha nyingi za pozi na mavazi mbalimbali.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post