YAMEZUNGUMZWA mengi juu ya sakata la staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny kuachana na mwandani wake wa sasa, Paula Paul au Paula Kajala na kurejea kwa mzazi mwenzake, Faima Msengi ‘Fahyma’, lakini Gazeti la IJUMAA limepewa ukweli wote.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kwamba, hadi anaondoka nchini kwenda masomoni nje ya nchi, Paula alikuwa akiishi na Rayvanny.
Hata wakati wa kuondoka nchini, Rayvanny alimsindikiza Paula hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Rayvanny ambaye ni Juma Lokole, Rayvanny hawezi kumuacha Paula na aliagana naye vizuri mbele ya mamamkwe wake ambaye ni mwigizaji Kajala Masanja.
“Rayvanny anajielewa, hawezi kurudi kwa Fahyma,” anasema Lokole.
STORI; MWANDISHI WETU, DAR
Post a Comment