Stan Bakora na Zee Cuty Wavuana Nguo Hadharani, Waweka Wazi Uchafu wao wa Chumbani




Baada ya msanii wa Bongo Flava, mrembo @zee_cuty kuvujisha siri za Ex wake ambaye ni mchekeshaji @stanbakora_ ,Stan pia karudisha mapigo kidizaini flani hivi.

Akiwa kwenye maiki za Refresh ya Wasafi Tv, Zee Cuty alidai aliachana na Stan Bakora kutokana na tabia zake,kwanza jamaa alikuwa analala na track suit pamoja na soksi akiulizwa kwanini,bwana mdogo anajibu anajitunza. 2. Stan ni mkoromaji usiku,3. Stan anaota ndoto akicheka usiku mzima,4. kwenye tendo akiwa anashusha mzigo anajimung'unya kama kameza ugali wa moto lakini pia ni mpenda majimama kila akimfumania anamfumania na majimama.

Kwa upande wa Stan Bakora akiwa kwenye kipindi cha Lavi Davi, Wasafi Fm amedai haoni kama kuna sababu za mtu kuzungumzia madhaifu ya Ex wake maana kuachana si uadui,vipi akisema Zee Cuty alikuwa analia kama mwewe kwenye tendo (kwa mfano😁). Kuhusu muda waliokaa kwenye mahusiano Stan amedai hawakudumu muda mrefu.

Huku akicheka, Stan amedai “uhusiano halijadumu lile,lilikuwa lina makolokolo mengi, uhusiano lilikuwa lina taharuki lile kwanza alikuwa ananielemea kiuchumi” 😁🙌

Sema kuvujisha siri za Ex wako sio mchongo kabisa.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post