MSANII wa Bongo Fleva, Snura Mushi maarufu kama Snura ametupa jiwe gizani..... Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Snura ameandika kifuatacho;
"Kuna Bibi anaitwa BIBI NGWENA a.k.a KIMYA KIMYA huyu bibi akishalewa na kuvuta miunga akachanganya na mibangi yake basi atakaekua mbele yake kaisha, atachambwa na kudhalilishwa hata kama hana kosa hii ilikua tabia yake kuwadhalilisha wenzie bila sababu kwa kujiona yeye ndio yeye waliobaki wote mangedele Ila watu wanakaaga kimya wanamuona HAMNAZO.
Sasa siku moja wakati anakuja MZEE SHIBE akasema ngoja leo nimtekenye yeye kidogo tuone atafanyaje weeeeeeeee alivyo tekenywa tu badala ya kucheka kaanza kulia majirani wakajaa wambea wakaanza kumuuliza kafanyaje kila mtu sasa akaanza kumuhoji.
Ila watu wengi walimpuuza kwasababu wanamjua mtu wa sifa alafu Hana dogo kama bomoa bomoa vibanda, basi Yule Bibi NGWENA akawa anajieleza kua yeye ni mzawa anajulikana ana watu wengi wanaomjua kuliko MZEE SHIBE kwanini amtekenye mbele za watu,,, kasahau kua Mzee SHIBE kamkuta,, kwenye kile kijiji yeye muhamiaji tu.
Kuna mtu akamwambia kama wewe mzawa na unajulikana sana mbona unafanya vitu vya hovyo hovyo kila siku unautumia vibaya huo uzawa mara unavamia nyumba za watu bila kuitwa mara unachamba watu unawadhalilisha unakua kama mgeni anaetaka kujulikana yani huendani na huo uzawa wala kujulikana kwako, Bibi NGWENA aliendelea kulalamika kua kadhalilishwa kasahau kabisaaaaaaa kama yeye ndio tabia yake PENDWA.
Watu wakamshukuru sana Mzee SHIBE Kwa alichofanya huenda kitamfanya bibi NGWENA kupunguza mihemko ili aendane na huo uzawa na kujulikana kwake au akahisi kidogo maumivu ya watu aliowadhalilisha.
#MuoshaHuoshwa na hii ndio hadithi ya BIBI NGWENA a.k.a KIMYA KIMYA" ameandika Snura.
Unadhani Snura amemlenga nani kwenye ujumbe huu?
Post a Comment