Siri ya Uzuri wa Zari Hassan Yagunduliwa..Kumbe Nusu Mhindi, Nusu Msomali




MWANAMAMA Zari The Boss Lady amefichua jambo ambalo wengi hawalijui kuwa, yeye ni mchanganyiko wa nusu Mhindi na nusu ni Msomali.

Zari ambaye ni raia wa Uganda amekuwa mgumu mno kuzungumzia asili ya wazazi wake. Mara chache aliwahi kuposti picha za mama yake, lakini hakuwahi kumuelezea kiundani.

Wengi wanamfahamu Zari kama mwanamke tajiri anayeishi nchini Afrika Kusini na ni mzazi mwenza wa mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz, lakini ukweli ni kwamba ana simulizi nyingi kuhusu maisha yake hadi hapo alipo.

Lakini hivi karibuni alifungua macho wafuasi wake zaidi ya milioni 9 kwenye Instagram baada ya kuwatonya kuwa, wazazi wake ni mchanganyiko wa Wahindi, watu wa Burundi na mchanganyiko wa Uganda na Somalia.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post